Friday, April 18, 2014

BARABARA KUU ILIyOZOLEWA NA MAFURIKO SASA INAPITIKA

Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi la Tanzania wamefanikisha kuifungua barabara ya Kongowe kuelekea Mjimwema hadi Kigamboni ambayo ilijifunga kutokana na kukatika kwa kalvati (PICHANI)katika mto Mtokozi. Kalvati hilo lilibomolewa na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa hapa jijini.

Hapo jana siku ya Jumanne, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pia alishirikiana na watendaji kwa siku nzima akiwa eneo la Mpiji kuhakikisha barabara ya Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo inaanza kupitika tena baada ya kuwa imejifunga kwa takriban siku tatu. Sehemu hii ya barabara iliathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha hivi karibuni. Matengenezo katika daraja la Mpiji yalikamilika jana usiku na magari yameanza kupiti bila ya matatizo.


Siku ya Jumatatu daraja jingine katika katika mto Kizinga kwenye barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Kongowe ilifunguka baada ya kazi ya usiku kucha iliyoongwozwa na Waziri Magufuli kufanikisha kukamilisha matengenezo katika sehemu hiyo yenye magari mengi. Barabara ya Kilwa ndiyo kiungo kikuu cha usafiri wa barabara kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini.

Aidha katika siku hiyo hiyo ya Jumatatu, daraja la Ruvu pia lilianza kupitisha bagari baada ya sehemu ya barabara iliyokuwa imeharibika kutokana na mafuriko, kukarabatiwa.

TAFAHDALI TO A MAONI YAKO



No comments:

Post a Comment