Mahakama moja imeatoa uamuzi kuwa kupiga picha watu za nguo
za ndani kwa kupiga chabo (utaratibu unaojulikana kama “upskirting”) bila ridhaa ya mhusika
sio kosa kisheria wakati akijibu suali muendesha mashtaka aliyetaka sheria hiyo
iangaliwe upya.
Mchezo huo ni kama ule wa kupiga chabo kwa kuweka kioo chini alafu kuangalia
msichana atakaesimama hapo bila kujua ili kuona nguo yake ya ndani.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na CNN leo, Mahakama Kuu ya
Massachusett ilipitisha uamuzi huo jana(jumatano) kwamba sio kosa kumchungulia
na kupiga picha nguo ya ndani ya mtu bila yeye kujua.
“abiria wa kike ambaye amevaa sketi au gauni au nguo
nyingine kujisitiri sio sawa na mtu aliye “nusu uchi” bila kujali kilichopo au
kisichopo chini ya sketi ikiwa kama nguo ya ndani au nguo nyingine” iliandikwa
na Jaji Margot Botsford wa mahakama ya rufaa.
Mchambuzi wa sharia wa CNN, Sunny Hostin alisema kuwa sharia
hiyo imepitwa na wakati kwani haiendani na teknolojia ya kisasa na kwamba ni
udhalilishaji wa wanawake na faragha.
Uamuzi huo ulitokana na kesi inayomshtaki Michale Robertson,
32 aliyekamatwa mwaka 2010 akidaiwa kutumia simu yake ya mkononi kupiga picha
na kurekoidi video wanawake.
Hata hivyo Robertson atahukumiwa kwa makosa mengine ambayo
adhabu yake yaweza kuwa ni mpaka miaka 2 jela akipatikana na hatia.
No comments:
Post a Comment