Akizungumzia ajali hiyo kwa njia ya simu jana, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa,Christopher Kangoye, alisema ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa tisa usiku eneo la Gulwe katika Wilaya ya Mpwapwa.
"Treni ilikuwa na mabehewa 20 kati ya hayo mabehewa 11 yalikuwa ya mafuta ya petroli na dizeli na mabehewa tisa yalikiuwa na mizigo mbalimbali na treni hiyo ilipofika katika eneo la Gulwe eneo ambalo mwaka jana reli ilichukuliwa na maji ikasombwa na maji ikapinduka"alisema Kangoye.
Aliongeza kuwa baada ya kupinduka kichwa cha treni kilisombwa na maji meta 100, mabehewa manne yalisukumwa moja likaanguka na mengine yakasombwa na maji. Alisema majeruhi wa ajali hiyo wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa na kwamba tayari watu wa reli wameshafika katika eneo la ajali jkwa ajili ya hatua zaidi
Aidha, alisema katika ajali hiyo inasadikika silaha mbili ambazo askari waliokuwa ndani ya treni hizo walizokuwa nazo zimepotea. Alisema inawezekana silaha hizo zimesombwa na maji kwa kuwa askari hao wasingeweza kuogelea nazo wkati ajalio hiyo ikitokea.
Alisema kila mwaka eneo hilo linafanyiwa matengenezo na mpaka jana lilifanyiwa marekebisho hivyo ni vyema litafutwa suhuhisho la kudumu ili kuondoa adha hiyo.
No comments:
Post a Comment