Ally Khatibu Haji (44) maarufu kwa jina la Shikuba, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, (JNIA) jumapili iliyopita baada ya kumsaka kwa zaidi ya miaka miwili.
Shikuba anajulikana kuwa ni muuza dawa za kulevya maarufu sana nchini na anafahamika kama kiongozi wa kundi la wauza dawa za kulevya nchini, inasemekana pia Shikuba ana mtandao mkubwa katika Afrika Mashariki, China, Brazil, Canada, Japan, Marekani na hata Uingereza.
Wiki iliyopita alishitakiwa kwa kusafirisha dawa zaidi ya kilo 210 za aina ya heroin zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 10 za kitanzania. Polisi walikamata mzigo wa dawa hizo mkoani Lindi mwezi januari 2012 ambazo zilihusishwa na Shikuba ambaye amekuwa mafichoni toka wakati huo.
Haijajulikana ni kwa jinsi gani aliweza kuingia nchini na kupata pasi mpya ya kusafiria, lakini tarehe 28 februari, polisi walifanikiwa kumkamata. Wapelelezi walimfuatilia Dar es Salaam kabla ya kumtega katika uwanja wa ndege akijiandaa kuondoka nchini.
Alikuwa uwanjani hapo kwa zaidi ya saa moja kabla polisi hawajamkamata saa saba mchana, ambapo alikuwa anajiandaa kuondoka kwa ndege ya South Africa. Mkurugenzi wa kitengo cha dawa za kulevya, Godfrey Nzowa alilithibitishia gazeti moja la kiingereza nchini, jana jumapili.
Ni kweli tumemkamata. Kukamatwa kwake ni mafanikio makubwa katika jitihada zetu za kulinasa mapapa hayo. Yeye ni mmoja wa washukiwa wenye nguvu na ushawishi mkubwa katika usafirishaji wa dawa hizo” alisema Nzowa.
Ni kweli tumemkamata. Kukamatwa kwake ni mafanikio makubwa katika jitihada zetu za kulinasa mapapa hayo. Yeye ni mmoja wa washukiwa wenye nguvu na ushawishi mkubwa katika usafirishaji wa dawa hizo” alisema Nzowa.
No comments:
Post a Comment