Monday, March 03, 2014

MKONGWE WA SOKA, KANU AFANYIWA UPASUAJI WA MOYO

Mcheza soka na super star wa Nigeria ambaye pia ni mwanzilishi wa KANU HEART FOUNDATION (KHF), Nwankwo Kanu, ambay pia ni Balozi wa Hisani wa UNICEF, amefanyiwa upasuaji wa moyo nchini Marekani katika hospitali ya Cleveland, Ohio.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa KHF, Mchungaji Onyebuchi Abia, upasuaji huo ulifanyika katika kipindi ambacho alitakiwa kufanyiwa uchunguzi ambapo kila mwaka hufanya hivyo.

Kanu amekuwa akifanyiwa chekup katika hospitali hiyo toka mwaka 1997, matatizo ya moyo. Kanu anatarajiwa kurudi nyumbani siku chache zijazo kutokana na hali yake kuendelea kuwa nzuri.



No comments:

Post a Comment