Akitoa ushahidi kwa mara ya kwanza, Mchina huyo alielezea mahakama ya Canada jinsi alivyoangalia kwa hofu kupitia mawasiliano ya Skype, huku aliyekuwa mpenzi wake alivyo shambuliwa na kuuawa katika nyumba yake huko Toronto, mji mkuu wa Canada.
“Wakati Qian Liu(KUSHOTO) aliposukumwa chini, niliona mguu wake. Ulikuwa unatingishika. Alikuwa bado anasema ‘No’kwa lugha ya Cantonese,” alisema Xian Chao Meng (KULIA JUU PICHA NDOGO)kwa Kichina huku mkalimani akitafsiri, liliripoti gazeti la Toronto Sun.
Alikuwa anawasiliana naye kutokea Beijing kwa kutumia kompyuta (laptop) yake. Na yeye pia alikuwa kwenye laptop, akiwa Toronto, ambapo alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha York.
Brian Dickson(CHINI PICHA NDOGO KULIA), jirani yake Liu ambaye pia alikuwa wanasoma chuo kimoja, anashtakiwa kwa kesi ya mauaji ya Liu aprili 2011. Kesi imeanza kusikilizwa jumatatu, wiki iliyopita. Wiki moja kabla ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo, Brian alijaribu kukiri kosa ili apunguziwe mashtaka, lakini jaji alikataa.
Liu, 23, alikuwa anaongea na aliyekuwa mpenzi wake katika kamera ya mtandao aliposikia mtu anagonga mlango wa chumba chake katika jengo lililokuwa karibu na chuoni kwake.
“Aliniambia kuna mtu anagonga mlangoni, na kwamba anaenda kuangalia. Kisha akafungua, na mwanaume mmoja “sio Mchina “ akatokea, Meng alieleza kwa mujibu wa gazeti la Sun. Waliongea kidogo na ndio Liu akampa simu yake ya mkononi. Anaonekana kubonyeza bonyeza kama anamtengenezea simu hiyo.

(PICHA: Kulia juu ni wazazi wa marehem Qian Liu wakiwasili mahakamani kusikiliza kesi ya mauaji ya binti wao.)
Liu, 23, alikuwa anaongea na aliyekuwa mpenzi wake katika kamera ya mtandao aliposikia mtu anagonga mlango wa chumba chake katika jengo lililokuwa karibu na chuoni kwake.
“Aliniambia kuna mtu anagonga mlangoni, na kwamba anaenda kuangalia. Kisha akafungua, na mwanaume mmoja “sio Mchina “ akatokea, Meng alieleza kwa mujibu wa gazeti la Sun. Waliongea kidogo na ndio Liu akampa simu yake ya mkononi. Anaonekana kubonyeza bonyeza kama anamtengenezea simu hiyo.
ENDELEA KUSOMA. . .
Kisha wanaonekana kuagana wakati “ghafla, kitu cha ajabu kilitokea”Meng aliiambia mahakama.
“Mwanaume huyo alijaribu kuingia ndani kwa nguvu. Liu alijitahidi kumzuia kwa kusukuma mlango, alishindwa na akaingia. Alijaribu kumkumbatia Qian Liu. Muda wote alikuwa (Liu) akijaribu kumsukuma kifuani”alisema
Kulikuwa na purukushani ambayo aliiona Meng. “Qian Liu akabanwa” alisema. Ilipofikia hapo alishindwa kuvumilia kutoa ushahidi. “Naomba muda kidogo tafadhali”alimuomba Mheshimiwa Jaji wa Mahakama ya Ontario, Anne Molloy.
Akiendelea kutoa ushahidi, alisema wote wawili walipotea kwenye mdanao wa kamera. Aliona mguu yake unatingishika huku akimsikia akiendelea kusema hapana. Akabadilisha toka Kingereza na kusema kwa lugha ya Kichina ya Cantonese, lakini mshambuliaji wake hakuacha.
“nilisikia vishindo viwili vya nguvu, tokea hapo sikusikia tena sauti ya Qian Liu”kilichofuata ilikuwa ni picha ya mwanaume akiwa uchi akiinama kuzima kamera ya mtandao wa Skype.
Meng aliposti taarifa kwenye mtandao aliojua Liu anatumia mara nyingi, akiomba mtu kwenda kumuangalia kwani maisha yake yalikuwa hatarini. Siku moja baadae, akasikia taarifa kuwa ameuawa. Mchunguzi alidai kuwa alikufa kwa kukosa hewa.

No comments:
Post a Comment