Tuesday, March 25, 2014

HII INATISHA SANA, WANAWAKE 4000 HUFARIKI DUNIA

Iringa
Wanawake 4000 nchini hupoteza maisha kila mwaka kwa ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi kila mwaka ambapo ni sawa na wastani wa wanawake11 kwa siku.

Mkurugenzi mtendaji wa mradi usio wa kiserikali T-MARC Tanzania Bi Diana Kisaka alisema leo katika ufunguzi wa mradi wa kuzuia na kudhibiti saratani ya mlango wa kizazi mkoani Iringa.

SOMA ZAIDI . . .
Alisema kuwa inakadiliwa kuwa kila mwaka wanawake 6000 hugundulika kuwa na ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi huku wanawake 4,000 wakifariki kila mwaka ikiwa ni sawa na wanawake 11 wanaofariki kila siku.

Hata hivyo alisema kuwa takwimu kutoka Hospital ya Ocean Road zinaonesha kuwa asilimia 40 ya vifo hivyo vinavyotokana na matatizo ya saratani ni wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ,

Aliongeza kuwa takwimu hizo pia zinaonyesha kuwa asilimia 80 ya wagonjwa wote wanaokwenda kwenye matibabu ya saratani ya mlango wa kizazi hufika Hospital kupata huduma hiyo kwa kuchelewa zaidi.

No comments:

Post a Comment