Chris Brown ameripotiwa kumbwaga mpenzi wake Karrauche huku akidaiwa kutaka kurudiana na mpenzi wake wa zamani, msanii maarufu Rihanna. Ripoti zinasema kuwa hii ilitokana na wivu ambao Chris ameshindwa kujizua kwa wasiwasi kuwa Rihanna sasa anarudiana na Drake ambaye ni adui yake mkubwa.
Mtandao wa Rada online umeripoti kwamba Chris alianza kumtumia Rihanna ujumbe wa simu kuanzia tarehe 20 februari, ambapo ilikuwa ni siku yake ya kuzaliwa na ndipo Karrauche alipoanza kuweka jumbe hizo katika mtandao wa Instagram na twitter, na kuacha kumfuata Rihanna katika mitandao ya kijamii.
“muheshimu mwanamke wako” bila kujali kuwa Karrauche amekuwa akimjali katika kipindi cha matatizo yake, mawazo yake bado yamekuwa kwa Rihanna. Kama unakumbuka katika siku ya kuzaliwa ya Rihanna, mama yake Chris pia alimtumia ujumbe wa kumtakia heri na kumita ‘Angel’ Malaika. Alilalamika Karrauche.
No comments:
Post a Comment