Mwanamke mmoja raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 36,
Sonia Perez Llanzon (PICHANI), amefariki dunia hivi karibuni baada ya kujiingizia kwa
kutumia bomba la sindano Vaseline kwenye matiti yake ili yawe makubwa.
Kwa mujibu wa gazeti la New York la Daily News, ambalo lilikariri vyombo vya habari vya Argentina, Sonia ambaye pia ni mzazi, alifariki wiki iliyopita baada ya kujichoma Vaseline. Sonia alilazwa hoaspitali kwa matatizo ya kupumua na ghafla akapatwa na tatizo la damu kwenye mapafu, alieleza Julio Pla,
Tukio kama hilo ni nadra sana japokuwa inadaiwa alijifanyia mwenyewe bila kupata msaada wowote kutoka kwa mtu yoyote.
Tukio kama hilo ni nadra sana japokuwa inadaiwa alijifanyia mwenyewe bila kupata msaada wowote kutoka kwa mtu yoyote.
Llanzon ameacha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 20,
mwanamke huyu aliyekumbwa na mkasa wa kusikitisha kwaajili tu ya kutafuta
urembo, inadaiwa aliona ni gharama au kutotaka kulipia gharama sahihi za
kutengeneza matiti yake kwa wataalamu wa shughuli hiyo.
SOMA ZAIDI . . .
Mkuu wa kitengo cha upasuaji katika hospitali ya Lucio Molas
alieleza,
“marehemu aliwasili hospitali akiwa na majeraha kwenye
matiti. Alikataa kila kitu mwanzo lakini baadae alikubali kwamba alijichoma
Vaseline kwenye matiti. Sijawahi kukutana na kitu kama hicho. Mwili wa
mwanadamu una askari wanaopambana na vijidudu na virusi lakini hauna namna ya
kuweza kupambana na bidhaa yeyote. Wengine kutumia Vaseline namna hii ni
kuhatarisha maisha”
Rafiki wa marehemu alisema, “hakuwa anapenda maumbile yake”
Kwa mujibu wa wataalamu kujichoma Vaseline kwenye uume au matiti
ili kukuza maumbile hayo ni hatari, kwani husababisha majeraha makubwa ambayo
huleta madhara makubwa kwa wanaume katika kusimamisha uume na kushindwa kufanya
kazi
No comments:
Post a Comment