'Sijui atapiga...' msimamizi wa maegesho ya magari Arusha akiangalia simu yake kwa makini huku maegesho hayo yakiwa yameegeshwa baskeli. |
'Ahh. . . Achana nae bana hana kitu huyo. . .' Askari polisi jijini Arusha wakimhoji dereva baada ya kumkamata juzi. |
Nguvu kazi, mzigo wa nguvu ukiwa kwenye mkokoteni jijini Arusha, nilifikiri hii ni style ya Dar peke yake, kumbe ni utamaduni wa Mtanzania. |
Caltural Heritage. . . kituo cha utamaduni cha Arusha kama kinavyoonekana. |
'Sijui leo itakuwaje. . .' Mama mchoma mahindi akitafakari jinsi atakavyopata wateja, wakazi wengi jijini Arusha wanafurahia sana mahindi ya kuchoma. |
Hii ndio helikopta ya kuelekea Loliondo, inasemekana inapiga ruti kama tatu hivi kwa siku. |
Inaelekea ng'ombe wa siku hizi wamekuwa 'mamwinyi' kama anavyoonekana mchunga ngombe akiwa na mzigo wa majani akipelekea wanyama wake |
'Kweli maisha ni magumu, duh...' kijana akitafakari huku akiwa amekalia toroli lake kama alivyokutwa jijini A-Town hivi karibuni |
'Kumbe DFP zina kazi nyingi eh...' jamaa wakiwa juu ya VX wanafunga tangzao katikati ya barabara jijini Arusha |
'Unakuja mjini na jembe, utalima lami...' wakijiandaa kuvuka barabara mama na mwanae katika jiji la Arusha hivi karibuni |
No comments:
Post a Comment