Friday, February 14, 2014

NANI ZAIDI LEO: UTAFITI KUHUSU VALENTINE NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Huu ni utafiti uliofanywa na shirika la Ipsos, utafiti huu ulilenga watu wenye umri wa zaidi ya miaka 18 katika miji mikubwa ya nchi tatu za Tanzania, Kenya na Uganda ili kujua uelewa kuhusu suala zima la siku ya Mtakatifu Valentine.

Walio hojiwa ni jumla ya watu 528 kutoka Tanzania, 1,050 Kenya na Waganda 1,006. Utafiti ulihoji watu wa jinsia zote yani wanawake na wanaume. Mahojiano yalifanywa kwa kutumia msaada wa computer na simu (CATI - Computer Aided Telephonic Interview) katika nchi hizo 3. utafiti huu ulifanywa kati ya tarehe 7 mpaka 10 mwezi februari, 2014


KUSHOTO: Jedwali la kwanza linaonesha umuhimu(kushoto) wa siku ya wapendanao na nia ya kusherehekea(kulia) siku hiyo


KUSHOTO : Tanzania kwa ujumla wake na nia nzima ya kusherehekea katika mgawanyiko tofauti, kumbe wanaume ndio wanania ya kusherehekea kuliko inavyofikiriwa kuwa wanawake ni zaidi.






KULIA: Katika nchi hizi 3 Tanzania ndio inaelekea wanatunaini kuwa siku hii itakuwa ya mashamsham ya mapenzi zaidi kuliko nchi nyingine.

Jedwali juu linaonesha jinsi matumizi yatakavyokuwa na pamoja na nchi zinavyotegemea kutumia pesa kwaajili ya siku hii. Watanzania wanategemea kununua nguo kuliko vitu vingine wakati Uganda na Kenya wanategemea kununua maua zaidi.




No comments:

Post a Comment