Rais Yoweri Museveni aliwaambia wanachama wa chama chake ijumaa iliyopita kuwa atasaini sharia hiyo ambayo itakuwa ni sharia kali kupinga ushoga ambayo itahusisha hukumu ya maisha.
Rais Museveni alijiridhisha na kuwa tayari kusaini muswada huo ili kuwa sharia kamili baada ya kupewa matokeo ya utafiti wa kisayansi kuwa ushoga sio suala la kuzaliwa nalo bali ni la kuiga ukubwani.
Kwa mujibu wa Amnest Intenational (shirika la kutetea haki za binadamu), ushoga ni kinyume cha sharia katika nchi 38 kati ya nchi 54 barani Afrika.
Vitendo vya kishoga vinaweza kusababisha hukumu ya kifo katika nchi kama Mauritania, Somalia ya Kusini, Sudan na Kaskazini Nigeria ambapo hukumu hutekelezwa kutokana na sharia za Kiislam.
No comments:
Post a Comment