Monday, February 17, 2014

MAREKANI YAMCHIMBA MKWARA MZITO MUSEVENI

Rais wa Marekani Barrack Obama amemwonya rais wa Uganda,Yoweri Musuveni, kwamba ikiwa atasaini mswada wa sheria inayoharamisha mapenzi ya jinsia moja basi uhusiano kati ya Uganda na Marekani utatatizika.

Chini ya sheria hiyo iliyopendekezwa, watu watakaopatikana na hatia ya kujihusisha na vitendo vya ushoga watakabiliwa na hukumu kali, ikiwemo kifungo cha maisha jela.

Marekani ni mojawepo wa mataifa ya kigeni yanayotoa kiwango cha juu zaidi cha msaada kwa Uganda, na mwaka 2011 idadi ndogo ya wanajeshi wa Marekani walitumwa kulisaidia jeshi la Uganda kupanda na kundi la waasi wa Lords Resistance Army, LRA.
Lakini Rais Obama amesema uhusiano huo unaodhaminiwa sana utatatizika zaidi iwapo mswada huo wa kupinga mapenzi ya jinsia moja utaidhinishwa na kuwa sheria.

Ameeleza kwamba mswada huo ni wa kidhalimu na hatari kwa jamii ya mashoga nchini Uganda.

Mshauri wa maswala ya usalama nchini Marekani, Susan Rice, amesema kwenye mtandao wa Twitter kwamba amefanya mazungumzo ya kina na rais Museveni jumamosi usiku kumtaka asitie saini mswada huo.

Mbali na Uganda rais Obama amelalamika kwamba visa vya mashambulizi na kuhangaishwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja vimeenea katika mataifa kadhaa kutoka Urusi hadi Nigeria.(BBC)

No comments:

Post a Comment