Siku chache tu baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museven kusaini ili kuidhinisha sharia mpya ya kupinga ushoga na shughuli zinazohusiana na ushoga, gazeti moja nchini humo limechapisha orodha ya “mashoga 200” raia wa nchi hiyo siku ya jumanne wiki hii.
Gazeti la Red Pepper, linalofanya shughuli zake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Kampala, limechapisha orodha ndefu ya majina, huku wengine wakiwa na picha zao chini ya kichwa cha habari “EXPOSED” (waanikwa).
Katika taarifa hiyo pia kuna jina la mchungaji wa kanisa katoliki, msanii wa muziki wa hiphop, na mwanaharakati maarufu wa ushoga nchini humo, Pepe Julian Onzieme. Inadaiwa baadhi ya waliotajwa humo hawakuwahi kujitangaza kuwa ni mashoga.
Taarifa hiyo imekuja muda mfupi tu baada ya serikali ya Uganda kutangaza sharia mpya ambayo inafanya shughuli zote za ushoga kuwa ni kosa.
Pamoja mataifa mbalimbali duniani kupiga vita hatua hiyo iliyopitishwa Uganda na vitisho mbalimbali vya nchi ya Marekani kwa Uganda vya kukata misaada, Rais Yoweri Museveni alisisitiza kuwa ni muhimu pamoja na kuingiliwa mambo yake na nchi za magharibi.
Museveni alikaririwa jumatatu akisema “Nini..!, wanafanya(mashoga) mambo ya ajabu” na kueleza kuwa wanatia “kinyaa.”
No comments:
Post a Comment