Tuesday, February 18, 2014

MAJANGA: AJITOA SADAKA KWA CHUI, AOKOLEWA KABLA YA KUTAFUNWA


Wafanyakazi wa zoo (eneo la kuhifadhi wanyama) huko China wamefanikiwa kuokoa maisha ya mtu ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili baada ya kutangaza kuwa anataka kuwaongeza afya ya chui waliofungiwa katika zoo hiyo kwa kujitolea mwili wake kama kitoweo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Yang Jinhai, 27, aliandika kwenye mitandao ya kijamii jinsi anavyojiandaa kuanza maisha mapya baada ya kupata kazi ya ulinzi Chengdu, kusini magharibi mwa China katika jimbo la Sichuan.
Lakini muda si mrefu baada ya kuanza kazi hiyo aliacha baada ya kuona kazi hiyo haimfurahishi na kuingia kwenye kiwanda cha uchapaji ambapo pia hakukaa na kuamua kuacha, akidai kuwa kuna mambo ya muhimu zaidi ya kufanya maishani.
Baada ya kutembelea zoo, aliandika jinsi ambavyo “chui wenye hadhi ya juu” wanavyoishi kwa unyonge wakiwa wamezungukwa na mazingira ambayo wamefungiwa na kushindwa kuishi kama asili yao ya uwindaji na kuua.
Na ndipo alipotangaza nia yake ya kujitoa sadaka ili awasaidie chui hao wanaojulikana kama Bengal Tiger.

PICHA NA STORY ZAIDI...
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Feng Lin alisema: “alipanda na kurukia ndani akitegemea, nafikiri, chui wangemrukia. Badala yake chui hao dume na jike wakashtushwa na kitendo hicho na jike likakimbia”
“Akaendelea kuwasumbua chui hao kwa kuwatishia, na ndipo chui dume akamrukia na kumrarua kwa makucha na kung’atwa kabla hajaokolewa na mhifadhi ambaye alimpiga risasi ya usingizi chui huyo.”
Familia ya Yang waliviambia vyombo vya habari kuwa Bw. Jinhai amekuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu na kudai amepelekwa nyumbani ambapo anatibiwa na wanasaikolojia jinsi ya kupambana na matatizo yake.


No comments:

Post a Comment