Tuesday, February 18, 2014

INATISHA :NYAMA YA BINADAMU YAUZWA HOTELINI, 11 WAKAMATWA

Alhamisi iliyopita polisi walikamata watu 11, baada ya kukuta vichwa 2 vya watu  katika hoteli (jina limehifadhiwa ) iliyoko karibu sana na soko maarufu la Ose-Okwodu, katika jimbo la Anambra, Nigeria.

Kwa mujibu wa gazeti la OSUN DEFENDER, katika tukio hilo pia zilikamatwa bunduki 2 aina ya AK47 pamoja na silaha nyingine kadhaa katika hoteli hiyo. Tukio hilo lilifuatia polisi kupewa tip na wakazi wanaoishi karibu na hoteli hiyo.

Mmiliki wa hoteli, wanawake 6 na wanaume 4 walikamatwa. Polisi walipovamia hoteli hiyo walikamata vichwa viwili vikiwa vimefungwa katika mifuko ya plastiki, bunduki 2 aina ya AK47, kofia 2 za jeshi, pamoja na silaha 40 za mauaji na simu kadhaa za mkononi.


“Kila ninapokuja sokoni, sababu hoteli iko karibu sana na soko, huwa naona mambo ya ajabu ajabu nje na ndani ya hoteli hiyo. Watu wachafu na tabia mbaya ndio wanaingia na kutoka katika hoteli hiyo.

Hivyo wala sikushangaa polisi walipogundua jana mapema tu asubuhi” alisema muuza mbogamboga katika soko hilo.

Mchungaji ambaye ni mmoja wa watu wailoidokeza polisi siku ya Alhamisi, alisema: nilienda kwenye hoteli hiyo mapema mwaka huu, baada ya kula, niliambiwa kuwa kipande kidogo tu cha nyama hiyo kinauzwa N700(sawa na shilingi za kitanzania 8000), nikashangaa. Kwa hivyo sikujua kama ni nyama ya mtu nimekula kwa bei ya juu kiasi hicho”





No comments:

Post a Comment