Wednesday, February 26, 2014
HUYU DADA ANAJIVUNIA NDEVU, ANA NYINGI KULIKO WANAUME
Siku hizi suala la kina mama kuwa na ndevu ni jambo la kawaida, lakini hii inashangaza kuona mwanamke ana ndevu nyingi kuliko mwanaume. Harnaam Kaur ni msichana wa miaka 23, mwalimu nchini Uingereza, tofauti na wasichana wengi yeye anajivunia kuwa na ndevu.
Msichana huyo (pichani) amekuwa na hali hiyo kwa lugha ya kitaalamu ‘polycystic ovary syndrome’, hali inayomfanya mwanamke kuwa na nywele nyingi kama au kuliko mwanaume.
Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la Daily Mail, Harnaam Kaur alianza kuota nywele usoni akiwa na umri wa miaka 11 jambo ambalo halikumfurahisha, alijaribu kuzinyoa, kubadilisha rangi ya uso wake kwa kujichubua lakini haikusaidia.
Shuleni, alinyanyaswa, aliitwa majina kama manywele, “jike-dume”. Ilifikia hatua ya kuogopa kutoka chumbani kwake, na kutaka kujiua.
Alipofika miaka 16, Harnaam mwenye asili ya India, alibatizwa na kuwa Singa na kwa sababu ya kipengele kimojawapo cha dini hiyo cha kuacha nywele zijiotee mwilini, Harman aliacha kuzikata nywele zake.
Mwanzo wazazi wake walipinga uamuzi huo, lakini Kaur alichoshwa na kuuficha uhalisia wake, alieleza “hivi ndio nilivyo, nipo tofauti na nimejifunza kujikubali moja kwa moja”. Kwa sasa Kaur amewekea mkazo uhalisia wake wa kike kwa kuvaa sketi, magauni na vito. Lakini bado anajaribu kuiangalia hali hiyo katika uchangamfu.
“Bado nikiingia dukani naitwa ‘bwana’ na kuonekana wa ajabu, ni ndevu zangu zinaonekana kwanza alafu ndio matiti. Ni jambo la linalochanganya watu wengi” alieleza Kaur. Shuleni ninapofundisha watoto wengi hunishangaa, baadhi huniuliza kwanini nna ndevu, na huwatania kuwa ni sare ya Halloween (sikukuu maarufu ya mizimu)”
Kraul alipata pendekezo la kuolewa toka kwa mwanaume, lakini anasema watu wanaume wengi katika jamii yao hawakubaliani na hali yake ya kuwa na ndevu.
“Bado sijapata mume, inanisikitisha... hali yangu inaonekana kuwa pingamizi ya ndoa, naamini bado nina muda wa kutosha kabla sijapata mume” alikaririwa katika kipindi cha televisheni ya Barcroft.
“Cha muhimu kwa sasa ni kujipenda, napenda ndevu zangu na vitu vingine – tattoo zangu, na kila kitu kwenye mwili wangu” alimaliza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment