Wednesday, January 08, 2014

WAKOLA AKAMATIWA SINGIDA NA RUNDO LA HELA FEKI

Singida.

Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mtu moja Toyi Wagela maarufu kama Wakola kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia 409 zenye thamani ya zaidi ya sh. 3/=.

Kamanda Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Geofrey Kamwela amebainisha kuwa mtu huyo ambaye ni mkazi wa mkoani Kigoma, alikamatwa na noti hizo akiwa katika Hotel ya Afro Petrol eneo la Chipondoda mjini Manyoni.

Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake jana Kamanda huyo alifafanua kuwa noti hizo ni pamoja na 200 za sh. 10,000/= na 209 za sh. 500/= ambazo zilipatikana baada ya kupekuliwa kutokana na mtu huyo kutoa noti moja y ash. 5,000/= kwa mhudumu huyo wakati alipokuwa anataka kulipia huduma ya chakula alichopata.

“Mtuhumiwa Tayi Wagela ambaye alikuwa mteja aliyekwenda katika hotel hiyo, ndipo aliposhtukiwa na mhudumu huyo na taarifa kupelekwa Kituo cha Polisi cha mjini Manyoni, ambapo askari wa jeshi hilo walikwenda huko na kumnasa akiwa na noti hizo". Alisema Kamanda Kamwela.

Jeshi hilo linaendelea kumuhoji mtu huyo ili kujua undani wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kina katika kubaini mahali zilipotengenezewa, watu wengine walioshiriki katika uhalifu huo wa utengeneza wa fedha bandia, na mtandao mzima unaotumika katika shughuli hiyo isiyo halali.

Kamanda alieleza kuwa mtu huyo atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika na kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na noti za bandia ambazo zinawezi kuwa katika mzunguko wa biashara mbalimbali mkoani Singida pamoja na kutoa taarifa ili hatua za kudhibiti ziweze kuchukuliwa na serikali kwa mujibu wa sheria.

No comments:

Post a Comment