Wednesday, January 29, 2014

MHINDI APIGWA NA WAHADHIRI WENZIE ST.JOSEPH UNI. SONGEA

ASINDIKIZWA DAR NA ULIZNI WA POLISI
ARUDI KWAO BAADA YA SHINIKIZO LA WANAFUNZI

Songea
Katika hali hisiyo ya kawaida siku chache zilizopita tangu wanafunzi wa chuo kikuu cha St. Joseph walipoandamana na kugomea masomo kwa lengo la kuushinikiza uongozi wa Chuo usitishe kuwavua nyadhifa na kuwasimamisha masomo rais wa serikali ya wanafunzi na waziri mkuu wake Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limelazimika kufungua jarada la uchunguzi kufuatia mhadhiri wa Chuo hicho raia wa India kushushiwa kipigo na wahadhiri wenzake ambao wanadai kuwa amewasaliti.

Habari zilizopatikana jana mjini Songea ambazo zimedhibitishwa na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ruvuma Deusidedit Nsimeki zilisema kuwa Mhadhiri huyo Robinson Nicolas ambaye alikuwa ni mshauri wa wanafunzi ( Muhadhiri) inadaiwa kuwa alishushiwa kipigo na wahadhiri wenzake janauari 23 mwaka huu, mchana.

Nsimeki alisema kuwa inadaiwa siku hiyo ya tukio Nicolas pamoja na wahadhiri wenzake wakiwa kwenye ofisi za chuo kikuu hicho ilitokea hali ya kutoelewana miongoni mwa uongozi wa chuo hicho dhidi ya mhadhiri Nicolas.

Mhadhiri Nikolas ambaye ni raia wa India pamoja na wahadhiri wenzake wakiwa wanaendelea kujadiliana kuhusiana na mgomo wa wanafunzi uliofanyika januari 21 mwaka huu ambao ulianza kwa maandamano na polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi.

Alifafanua kuwa katika kujadili wao wenyewe walianza kutuhumiana ambapo walimtuhumu Nicolas wakidai kuwa ndio alikuwa chanzo cha mgogoro huo kwani wanafunzi walipo andamana walibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe mbalimbali ambao ulionyesha wazi kuwa Nicolas alikuwa na lugha chafu kwa wanafunzi

Alisema kuwa kutokana hali hiyo uongozi wa Chuo hicho uliamua kusitisha ajira yake na kutokana na matatizo ambayo alionekana Nicolas ni Chanzo kuwa na lugha chafu kwa wanafunzi ambapo wanafunzi wenyewe wakati wa maandamano walibeba mabango yaliyoandikwa NICOLAS GO BACK TO INDIA.

Kamanda Nsimek alifafanua kuwa katika kumhoji Nicolas alieleza kuwa yeye ana msimamo hakukubaliana kabisa na uongozi wa chuo wa kutaka kuwasimamisha masomo wanafunzi 25 waliodaiwa kuwa ni sehemu ya wanafunzi walioleta mgomo.

Nicolas alieleza kuwa alipokataa kusaini barua za kuwasimamisha masomo wanafunzi ndipo alipoanza kushushiwa kipigo na baadae alifanikiwa kukimbia hadi kwenye nyumba ya jirani na Chuo ambako aliomba kujihifadhi lakini mmiliki wa nyumba hiyo mwalimu Deogratiasi Komba wa shule ya msingi London alikubali kumhifadhi na baadaye alimpeleka kwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya mtaa ambaye ndiye aliyetoa taarifa kituo kikuu cha polisi cha Songea kuhusiana na tukio hilo.

Kamanda Nsimeki alieleza kuwa Nocolas alishambuliwa na wahadhiri wenzake na kusababisha kuwa na michubuko sehemu za mguu wa kulia, mkono wa kushoto na kifuani.

Alisema kuwa hata hivyo juzi Nicolas alisafirishwa kwenda jijini Dar es salaam kwa kusindikizwa na polisi kwani alilazimika kuomba yeye mwenyewe ulinzi wa polisi na anatarajiwa kurudi kwao nchini India.


No comments:

Post a Comment