Songea
Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma linamshikilia Fikiri Mapunda (32) mkazi wa kitongoji cha
Msirikasi kilichopo kijiji cha Malunga
kata ya Tingi wilaya ya Nyasa kwa tuhuma za kumchoma kisu shingoni Yakobo Mbungu (29) mkazi wa kitongoji
hicho wakati wakinywa pombe za kienyeji ambapo alifariki muda mchache wakati akikimbizwa kwenye
hospitali ya Wilaya ya Mbinga kwa ajili ya matibabu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma
Deusdedit Nsimeke amesema tukio
hilo limetokea juzi majira ya saa nne
usiku kwenye klabu za pombe za kienyeji
,ambapo Marehemu na mtuhumiwa walikuwa wakinywa pombe ghafla walianza kurushiana maneno ambapo inadaiwa chanzo cha ugomvi huo ni wivu wa mapenzi.
Amefafanua zaidi kuwa, Yakobo anadaiwa alikuwa na mahusiano
ya kimapenzi na Vumi Kawonga ambaye kwa siku za nyuma kabla ajaanza kuwa na
mahusiano na mapunda alikuwa ni mpenzi wa
marehemu.
Ameongeza kuwa, siku ya tukio inadaiwa mapunda na Marehemu
walikutana kwenye hicho klabu ambapo
walianza kurushiana maneno na kila mmoja
alimtuhumu mwenzake kuwa alimuibia mpenzi wake
na baadaye ulizuka ugomvi mkubwa
kisha Yakobo alichomwa kisu na kumwaga damu nyingi ambazo zilisababisha
apoteze maisha.
Amesema, mara baada ya uongozi wa serikali ya kijiji kupata
taarifa za mauaji hayo ulimkamata mtuhumiwa na kumpeleka kwenye kituo cha
polisi cha Mbambabay ambapo anaendelea
kushikiliwa na Jeshi hilo hadi upelelezi wa polisi utakapokamilika kwa ajili ya
kumpeleka mahakamani.
No comments:
Post a Comment