Wednesday, January 22, 2014

ANGALIA VIWANJA VYAVYOVUTIA BRAZIL KOMBE LA DUNIA 2014

Kitu kimoja kinachoivutia FIFA kuhusu kombe la dunia la Brazil ni jinsi viwanja vyake vinavyong’aa na kuvutia wengi. Viwanja hivyo ambavyo vinatarajiwa kukamilika kabla ya kombe la dunia kuanza mwaka huu 2014, vingi vimeshaisha.

Blog ya IMMAMATUKIO imejaribu kutafuta sura za viwanja hivyo ili kukuweka wewe msomaji karibu na maandalizi hayo. Japokuwa hizi picah ni mpaka kufikia mwaka 2013, oktoba.

Tukio hili kwa Brazil bila kubisha ni kubwa sana, linasubiriwa na wapenzi wengi wa soka ulimwenguni.

Kila kiwanja kinatengenezwa kwa mtindo tofauti ili kuvutia kila atakaye weza kufika au hata kuona kwenye runinga yake. Angalia katika picha hizi 12 utakubaliana na mimi.

Tuanze…

JINA: Mineirao
MAHALI KILIPO: Belo Horizonte, Minas Gerais

KINACHUKUA WATU: 62,160

HUDUMA NYINGINE: MITA ZA

MRABA7,500, zaidi ya maduka100, bar na migahawa

HALI YAKE : Kimekamilika





JINA : Estadio Nacional Mane Garrincha

MAHALI KILIPO: Brasilia, Federal District

UWEZO: 72,788

HUDUMA NYINGINE: kimewekwa kwa mwelekeo ambao unaweza kupata jua na hewa ya kutosha kuendesha mashindano

HALI YAKE: Kimekamilika




JINA: Arena Pantanal
MAHALI KILIPO: Cuiaba, Mato Grosso

UWEZO: 43,600

HUDUMA NYINGINE: Maeneo mbalimbali ya mazoezi, maeneo asilia pamoja na ziwa na msitu wa mbao.

HALI YAKE: Bado hakijakamilika





ANGALIA PICHA ZAIDI...

JINA: Arena Da Baixada


MAHALI KILIPO: Curitiba, Parana

UWEZO: 42,000

HUDUMA NYINGINE: Uwezo wa kufunika juu uwanja mzima kuzuia mvua.

HALI YAKE: kinafanyiwa marekebisho





JINA: Estádio Castelao


MAHALI KILIPO: Fortaleza, Ceara

UWEZO: 63,903

HUDUMA NYINGINE: Kinazibwa na kioo laini chenye kupunguza miale ya jua na joto.

HALI YAKE: Kimekamilika





JINA: Arena Amazonia


MAHALI KILIPO: Manaus, Amazonas

UWEZO: 42,374

HUDUMA NYINGINE: Mfumo wa kutumia maji ya mvua na matundu ya kuingiza hewa asilia ili kupunguza matumizi makubwa ya umeme.

HALI YAKE: Bado hakijakamilika



JINA: Arena Das Dunas


MAHALI KILIPO: Natal, Rio Grande do Norte

UWEZO: 42,000

HUDUMA NYINGINE: Runinga mbili kubwa ndani ya uwanja na ziwa la kutengeneza nje ya uwanja.

HALI YAKE: Bado hakijakamilika





JINA: Estadio Beira-Rio


MAHALI KILIPO: Porto Alegre, Rio Grande do Sul

UWEZO: 51,300

HUDUMA NYINGINE: Paa lililotengenezwa kwa material maalumu ya polytetrafluoroethylene membrane ili kujisafisha na kutokunyonya uchafu.

HALI YAKE: kinafanyiwa marekebisho


JINA: Arena Pernambuco


MAHALI KILIPO: Recife, Pernambuco

UWEZO: 46,000

HUDUMA NYINGINE: Kinatumia umeme wa jua, maji ya mvua yanakusanywa kwa matumizi mengine na viti vyote vimezibwa na paa.

HALI YAKE: Kimekamilika



JINA: Estadio Do Maracana


MAHALI KILIPO: Rio de Janeiro, State of Rio de Janeiro

UWEZO: 78,000

HUDUMA NYINGINE: Hichi kiwanja kimebadilishwa na kutengenezwa upya kabisa, pamoja na kwamba muonekano wake uko vilevile, paa lake limezibwa lakini unaweza kuona nje na linashikiliwa na kamba maalumu.

HALI YAKE: Kimekamilika



JINA: Arena Fonte Nova


MAHALI KILIPO: Salvador, Bahia

UWEZO: 55,000

HUDUMA NYINGINE: Kina uwazi eneo la kusini mwa uwanja ili kuona mandhari ya chemchem za Tororo Dyke.

HALI YAKE: Kimekamilika





JINA: Arena Corinthians


MAHALI KILIPO: Sao Paulo, Sao Paulo State

UWEZO: 68,000

HUDUMA NYINGINE: Kimejengwa kwa ubunifu mkubwa na wa kutumia vyuma vingi.

HALI YAKE: Bado hakijakamilika







No comments:

Post a Comment