Tuesday, December 24, 2013

MUGABE AZIDI KUMSUTA TSZANGIRAI AMWAMBIA "KAFIE MBELE"

Rais Robert Mugabe kavunjilia mbali matumaini ya ushirikiano na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, kwa kusema wapinzani wa MDC-T na kiongozi wao “Wakafie Mbele”

Akiongea jumapili iliyopita akiwa Bulawayo alipokuw akizindua sanamu ya marehemu makamu wa rais Joshua Nkomo aliyefariki mwaka 1999, Mugabe aliwataka mashujaa wa vita kurudi ZANU PF.

“Simuongelei (Morgan) Tsvangirai na MDC; hao wakafie mbele. Nawaambia (mashujaa wetu) wanaopambana na maadui, hamuoni uchungu unaowapata watu” Mugabe alisema

“Vifo na majeraha yaliyowapata wakati wa mapambano na mnadiriki kushirikiana na adui wa watu wenu wenyewe? Naongelea kuhusu msimamo wa upinzani leo kugeuka na kukimbilia Waingereza na Wamarekani ili tu watupinge”

Aliweka mkazo kiongozi huyo wa ZANU PF.

“Hatujali upinzani ndani ya nchi. Lakini upinzani unao kwenda kumbembeleza, nchi zile zile zilizo tudidimiza, hiyo imepitiliza. Ni uhaini, ni uhaini wa ajabu sana” alisema

Zanu PF inamlaumu Tsvangirai kwa kushirikiana na waliokuwa wakoloni wa Zimbabwe wanaolazimisha kubadilisha serikali ya nchi hiyo. Lakini kiongozi wa MDC-T amekataa tuhuma hizo.

Mugabe aliwatembelea mashujaa hao ambao waliondoka Zanu PF, akiwataka warudi kwenye chama.

Aliyekuwa kiongozi wa ZIPRA Dumiso Dabengwa pamoja na wenzie waliokuwa na kinyongo walijitoa Zanu PF ili kurudisha chama cha PF Zapu katika uchaguzi wa mwaka 2008, ikiwa ni kwa sababu Bw. Mugabe alikataa kukabidhi nchi kwa viongozi wenye umri mdogo.

Mashujaa hao wa vita wakishirikiana na upinzani wanamdharau Nkomo alidai Bw. Mugabe.

“Jana aliwaambia (Nkomo) mrudi hapa. Sasa ameondoka mnafikiri sababu yuko kaburini hastahili heshma?”

“Hivyo nawaambia mashujaa, mlipigana vita moja dhidi ya adui, hata kama wewe ni Zipra au Zanla, rudini mnapostahili, msipotee. Hao (Mashujaa) ndio wanaonifanya nilie sababu hao wako chini yetu, chini ya uongozi wetu”

“hawakutakiwa kujitenga, wanatakiwa kuungana sababu ya wazo zima lililotufanya tupambane, hata kama tunaurafiki na Muungano wa Sovieti au China ilikuwa sawa tu. Tunaondoa mapungufu yetu kwa kukaa chini na kuongea” alimaliza Mugabe

No comments:

Post a Comment