Monday, December 16, 2013

MTOTO AMUUA DADA YAKE KWA KUIGA MIELEKA

Mtoto wa miaka 13 amehukumiwa kwenda jela miaka 3 kwa kumuua mdogo wake wa kike mwenye miaka 5.

Kijana huyo alimuua mdogo wake ikidaiwa alikuwa anajaribisha mtindo wa mieleka kwa mdogo wake huyo, msemaji wa mahakama aliiambia CNN katikati ya wiki iliyopita.

Inadaiwa kijana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kutokana na umri wake kuwa mdogo, aliachwa na mdogo wake huko New Orleans, nchini Marekani, mwezi juni, 2013, na kwamba mtoto huyo alijaribisha kwa dada yake style ya mieleka ya WWE aliyoiona kwenye sinema.

Hata hivyo mtoto huyo atapunguziwa adhabu sababu tayari amesha kaa jela.





No comments:

Post a Comment