Wednesday, September 04, 2013

MAHAKAMA YASITISHA KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI WAJAWAZITO


Hukumu ya hivi karibuni ya mahakama ya kikatiba imethibitisha kwamba shule haziwezi kuwafukuza wanafunzi kwa kupata uja uzito.Lakini Afrika Kusini bado inang'ang'ana kukabliana na suala hilo linalowaathiri wasichana 180,000 kila mwaka.

Daktari Jay-Anne Devjee ambaye ni mkuu wa afya ya akina mama katika hospitali ya King Dinuzulu anasema kwa mara nyingi hulazimika kuwazalisha wasichana kwa njia ya upasuaji, jambo linaloongeza hatari ya kuvuja damu na kuhatarisha maisha ya wazazi hao.

Phumla Tshabalala, mwenye umri wa miaka 16, anamshikilia mwanawe mchanga aliye na umri wa siku moja.Hii ni mara yake ya kwanza kujifungua na anasema ana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kumlea mwanawe peke yake.Msichana mwenye umri mdogo zaidi hapa ana umri wa miaka 14 na anaonekana kuzidiwa na uchungu wa uzazi kiasi cha hata kushindwa kuongea.

Anaeleza hajamuona mpenzi wake kwa muda mrefu na licha ya kumuarifu kwamba amejifungua, hakuna mtu kutoka familia ya mpenzi wake aliyekuja kumjulia hali. Anatoka katika familia maskini, Babake ndiye anayeilisha familia. Yeye ni binti wa mwisho kati ya mabinti watatu na wa kwanza aliyejifungua mtoto, jambo ambalo familia yake bado haijalipokea vyema.

Inakisiwa kuwa kila mwaka wasichana zaidi ya laki moja na themanini nchini Afrika Kusini hushika ujauzito. 180 kati ya wengine 1000, hupata kuwa wajawazito. 36% ya wasichana wenye mimba hufariki kila mwaka kulingana na takwimu za nchi hiyo wakati wanapojifungua.

Mifuko yao ya uzazi huwa bado haijakuwa vyema kiasi cha kubeba mimba na wengi huwa na wakati mgumu sana wanapojifungua , kulingana na daktari Jay-Anne Devjee.

Phumla anapanga kurudi shuleni kwa wakati muafaka ili aweze kufanya mtihani wa mwisho wa mwaka , lakini ana wasiwasi kuhusu vipi atakavyoweza kutimiza majukumu yote mawili ya kuwa mwanafunzi na mzazi pia.


No comments:

Post a Comment