Tuesday, September 24, 2013

KUNGUNI WAVAMIA BUNDA

WAKAZI  wa Kijiji cha Kunzugu  kata ya Kunzugu wilayani Bunda  wameiomba Idara ya afya kuwanusuru na uvamizi wa wadudu aina ya  Kunguni  katika nyumba zao zenye kaya 399.

Wakazi hao wametoa  ombi hilo jana kwa mbunge wa jimbo la Bunda Stephen Wasira katika mkutano wa adhara kijijini hapo  ambapo walieleza  kuwa kuna kunguni wa kutisha hasa baada ya idara ya afya  kunyunyuzi  katika nyumba hizo  dawa ya kuua mbu.

Walidai kunguni hao wamevamia nyumba zao na kuishi kwenye vitanda, mashuka, meza, viti, nguo na kila kona ya nyumba ambapo wametumia  kila njia ya kuwaangamiza  bila ufanisi.


Akitoa kero hiyo kwa niaba ya wenzake, Paulo Mwangwa mkazi wa Kijiji hicho aliishambulia wizara ya afya kwa madai kuwa kunguni wamesabishwa na  unyunyizaji wa dawa za mbu katika nyumba zao.

“Mheshimiwa mbunge wetu, kabla ya dawa hii ya mbukunyunyizwa majumbani  kwetu hatukuwa na
kunguni , sisi tulidhani dawa hii inaua wadudu wote kwa nini sisi imetuletea kunguni?alihoji Mwangwa akishangiliwa na wananchi wenzake.

Wasira aliagiza idara ya afya kufanya uchunguzi wa kuwepo kwa Kunguni hao huku Mmoja  wa mganga
kutoka idara ya afya wilayani humo aliyejitambulisha kwa jina la Kateire akidai  dawa ya kuangamiza mbu aina ya anopheles  uua wadudu aina zote hivyo watafanyia uchunguzi suala hilo.



No comments:

Post a Comment