BAADA ya kugundua kuwa biashara ya ukahaba inalipa kwa upande wao, wanawake wanaojishughurisha na biashara hiyo nchini Kenya waomba watambuliwe na wapewe ulinzi wanapokuwa kazini ili na wao walipe kodi kwa serikali, hatua hiyo itachangia biashara hiyo kutambulika rasmi.
Wanawake hao wametoa maombi hayo kupitia chama chao kinachojulikana kwa jina la Africa Sex Workers Alliance (ASWA) kinachopatikana nchini humo na kubainisha kuwa biashara yao ni sekta ambayo inatoa fursa nzuri kwa nchi kujiendeleza kiuchumi.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mkurugenzi wa chama hicho Doughtie Ogutu alisema chama hicho kilianzishwa kwa madhumuni ya kutetea maslahi ya wanachama ambao wamepitia mengi yakiwemo kupigwa kuuwawa na hata kulazimishwa kushiriki ngoni na wanyama.
"Tunataka watu watuangalie kama tunaweza kusaidia kukuza uchumi na wala si kuangalia kwamba tunaendeleza mmomonyoko wa maaadili" alisema.
Ingawa wanaamua kuendelea na biashara hiyo makahaba wanakiri kwamba biashara hiyo ni hatari hasa iwapo wanapata wateja wabaya .
Bi Ogutu alielezea kwamba anakumbuka miaka minane iliyopita mmoja wao alipopata mteja mzungu lakini akarejea akiwa maiti, tena mwanzoni mwaka huu wasichana wakakamatwa katika eneo la pwani wakiwa na mwanamume mwengine wa kigeni na kushtakiwa kwa kujihusisha na ngoni isiyostahili.
Kwa sasa chama hicho kinapanuka kutokana na kuwepo kwa mataifa kumi na kinaelekea magharibi na Afrika ya kati, lakini ushawishi nchini Kenya unakumbwa na changamoto nyingi.
No comments:
Post a Comment