Mzozo kati ya Cisse na klabu yake umetatuliwa
Papiss Cisse na wasimamizi wa
klabu ya Newcastle hatimaye wameafikiana na sasa mchezaji huyo ataanza
kuvalia sare rasmi ya klabu hiyo iliyo na nembo ya kampuni ya Wonga,
licha ya msimamo wake wa kidini.
Cisse, ambaye ni Muislamu, alijiondoa kutoka kwa
kikosi cha Newcastle kilichokwenda ngambo kwa mazoezi yake ya klaby ya
msimu kuanza, baada ya kuwafahamisha wasimamizi wa klabu hiyo kuwa
hakuwa tayari kuvalia sare ambayo inaendeleza kampuni ya kutoa mikopo.Lakini baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa muda wa wiki moja, pande hizo mbili zimeafikiana na Cisse sasa ataendelea kuichezea klabu hiyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka ishirini na minane anatarajiwa kurejea tena katika kambi ya Newcastle baada hii leo.
Cisse ni mmoja wa wachezaji wa Newcastle ambao ni Waislamu lakini ndiye mchezaji wa pekee ambaye alikataa kuvalia sare hiyo.
Nyota huyo wa timu ya taifa ya Senegal amekuwa akifanya mazoezi mwenye huku wachezaji wenzake wakiendelea na mazoezi yako nchini Ureno.
Oktoba mwaka uliopita, ilitangazwa kuwa kampuni inayotoa mikopo kwa riba ya juu ya Wonga, itakuwa mdhamini mkuu wa klabu hiyo msimu huu kuchukua mahala pa kampuni ya kutuma pesa ya Virgin.
Inaaminika kampuni kugharimu dola milioni nane.
Cisse alijiunga na Nedwcastle Januari mwaka wa 2012 na amefunga jumla ya magoli ishirini na sita
No comments:
Post a Comment