Tuesday, July 23, 2013

MSICHANA AIBA KADI YA BENKI KULIPIA GESTI.

msichana mwenye umri wa miaka 24 amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kuiba kadi ya benki ya mama yake na kutoa fedha alizotumia kulipia hoteli aliyolala na mtoto wa miaka 14.

Msichana huyu aliyetambulika kwa jina la Natalie Williams, mkazi wa Darlington, nchini Uingereza, alisema alilazimika kuiba kadi ya mama yake na kwenda kutoa pauni 1,000 (zaidi ya sh. milioni mbili ya kitanzania), ambapo aliweza kulipia hoteli yenye hadhi ya nyota nne alikolala na mtoto huyo.


Msichana huyu alieleza mahakama kuwa alilazimika kufanya hivyo baada ya kucheza na mtoto huyo na kupandwa na mihemko aliyoshindwa kuizuia.

Baada ya tukio hilo kufika mbele ya sheria, msichana huyo aliamua kumtafuta bwana aliyetembea naye na kumpa ujauzito ili kukwepa adhabu ya kwenda jela

Jaji Simon Bourne Arton wa Mahakama ya Darlington, alisema msichana huyo hawezi kukwepa jela kwani sheria imewekwa wazi kuwa yeyote anayetenda kosa la kutembea na mtoto awe mwanamke au mwanaume lazima akumbwe na adhabu hiyo

No comments:

Post a Comment