Friday, July 12, 2013

MALIPO YA WALIMU YAIUMBUA SERIKALI


Wakati serikali imetoa tamko juu ya limbikizo la deni linalodaiwa na walimu kuwa zaidi ya sh. bilioni 1.2, kama malimbikizo ya mishahara kati ya Julai 2012 na juni mwaka huu, madai ambayo yalipelekwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Rais wa Chama cha Walimu (CWT), Gratian Mukoba amekanusha juu ya madai hayo.

Akizungumza kwa njia ya simu Mukoba aliweka wazi kuwa madai yao yanafikia sh. bilioni 33 ikiwa ni malimbikizo ya mishahara pamoja na madeni mengine.


Aliweka wazi kuwa wakati wa migomo hapo awali walikutana na waziri mkuu Mizengo Pinda na aliwahidi kushughurikia tatizo hilo.

Alifafanua kuwa deni hilo limezidi kuongezeka kutokana na baadhi ya walimu kupandishwa daraja, hivyo mwalimu anapopandishwa daraja na mshahara wake unaongezeka

No comments:

Post a Comment