Mfanyabiashara Mmiliki wa Home Shopping Center (HSC), Said Mohamed Saad (Pichani), aliyemwagiwa tindikali wiki iliyopita katika shopping mall mpya ijulikanayo kama Msasani City Mall, jijini Dar es Salaam, yuko katika matibabu Afrika Kusini.
Bw. Saad alimwagiwa tindikali ikiwa ni kiasi cha wiki mbili tangu Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, mkoani Arusha, Said Juma Makamba naye ajeruhiwe vibaya usoni kwa kumwagiwa tindikali usiku nyumbani kwake.
Kumwagiwa tindikali sio jambo jipya nchini kwani ndani ya miaka miwili pekee, watu zaidi ya watano wameshamwagiwa tindikali nchini.
Vyombo vya habari nchini viliripoti wiki iliyopita tukio la mfanyabiashara huyo kumwagiwa tindikali ikiwa ni tukio lililotokea ijumaa tarehe 19 julai, ambapo saa moja jioni, mfanyabiashara Said Mohammed Saad alimwagiwa tindikali na mtu mmoja ambaye hakufahamika na mara,
Mhusika alikimbia huku mlinzi wa eneo hilo alimkimbiza lakini hakufanikiwa kumkamata baada ya kuteleza na kuanguka. Hatua hiyo ilimwezesha mtuhumiwa kutoroka eneo la tukio kwa kutumia pikipiki.
No comments:
Post a Comment