Wednesday, June 26, 2013

VIGOLI WAKUTANA KWA AJILI YA UTAMBULISHO


WASHIRIKI wa shindalo la kumtafuta Kigoli wa Tanzania kutoka katika mikoa ya Tanga pamoja na Morogoro wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi wa shindalo hilo linalotarajia kufanyika Juni 30 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mratibu wa shindano hilo Maimartha Jesse alisema kuwa washiriki kutoka mkoa wa Tanga, pamoja na Morogoro wamewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uzinduzi ambao watapatika washiriki 15 watakaoingia kambini.


Alisema kuwa kabla ya kufanya uzinduzi huo vimwana hao wanatarajia kufanya utalii wa ndani ikiwemo kutembelea makumbusho ikiwa ni mmoja ya kutangaza utalii wa nchi.

"Sasa hivi mashindano yamepamba moto kila mmoja anajichua kumshinda mwenzie hivyo wanafanya mazoezi ya kutosha kwa ajili ya kushindana kucheza na ndipo tutakapompata mshindi mmoja" alisema Maimatha.

Uzinduzi huo ambao unatarajia kufanyika Traventain Magomeni jijini Dar es Salaam huku muimbaji mkongwe wa taarabu Mzee Yusph akipamba uzinduzi huo kwa burudani ya kipekee.




No comments:

Post a Comment