Wednesday, June 26, 2013

GOSBY AWAJALI MABINTI


Msanii wa miondoko ya Hip Hop Gosby amefikiria kufanya kitu cha tofauti kwa ajili ya kuboresha muziki wake na kuamua kutoa  nafasi kwa wasichana watatu watakaoweza kujibu maswali yanayohusu muziki wake kwa ufasaha kwenda kusikiliza kwa mara ya kwanza wimbo wake mpya alioupa jina la 'Baby Making Swag aka BMS' siku ya Jumatano (leo) kwenye studio za B'Hits zilizopo Kawe.


Aliweka wazi kuwa ameamua kuwachagua  wasichana pekee yake kwa sababu mahadhi na ujumbe unaopatikana kwenye nyimbo hiyo unawagusa wasichana zaidi.

Mbali na hilo pia ameamua kuwafanya wasikilizaji wake kuwa wa kwanza kuusikiliza muziki huo, huku akitarajia kupata ushauri kupitia mashabiki wake.





No comments:

Post a Comment