Baraka Obama
atawasili leo nchini Afrika ya Kusini na kutegemewa kutembelea mahali alipokuwa
anaishi rais wa kwanza wa taifa hilo ambaye yuko maututi kitandani kwa matatizo
ya kupumua.
Rais Obama
na Bw. Mandela ambaye wanatarajiwa
kukutana na kwa muda usiojulikani na kuishia kupiga picha tu.
Kutokana na
afya ya Mandela kuwa mbaya, wawili hao hawatarajii kukaa muda mrefu hata mbele
ya kamera za waandishi wa habari.
Rais huyo wa
kwanza mweusi wa Afrika Kusini ambaye atatimiza miaka 95 mwezi ujao,
alikimbizwa hospitali wiki tatu zilizopita akiwa na matatizo ya mapafu.
Afya ya Bw
Mandela imezidi kuwa mbaya siku chache kabla ya ujio wa Obama nchini Afrika
Kusini, lakini pia hali hiyo haijabadilika na kusababisha Rais Jacob Zuma kufuta
ziara yake nchini Msumbiji.
“anaendelea
vizuri sana leo” alidai Bw. Zuma baada ya kumuona Mzee Mandela jana jioni ikiwa
ni mara ya pili katika kipindi kisichozidi masaa 24.
Raia wa nchi
hiyo wamekuwa wakimuombea Mzee Nelson ‘Madiba’ Mandela katika sala zao aendelee
kupona.
"Siwezi
kudanganya, hali sio nzuri” alisema mtoto wa kike wa Mzee Mandela, Makaziwe
Mandela. "tukiongea naye anajibu na
kujaribu kufungua macho-bado tunaye”
"Lolote
laweza kutokea, lakini ningependa kusisitiza tena kwamba ni mungu tu ndio
anajua ni saa ngapi ataondoka” aliiambia radio moja nchini Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment