Saturday, June 29, 2013

OBAMA KUKUTANA NA FAMILIA YA MANDELA

KUTOKWENDA HOSPITALI KUMUONA MZEE MANDELA



Rais Obama akipokewa katika uwanja wa ndege wa Waterkloof, nchini Afrika Kusini mapema leo

PRETORIA | Sat Jun 29, 2013 4:07am EDT 

Rais Onama wa Marekani akiambatana na mkewe, Michelle Obama watakutana leo na ndugu wa Nelson Mandela. Kama ilivyotarajiwa Rais Obama hatokwenda hospitali alikolazwa Bw. Mandela kama ilivyoelezwa mwanzo


Taarifa kutoka Ikulu ya White House ya Marekani, zimedai kuwa Bw. Obama hatokwenda hospitali hapo ambapo amelazwa akiwa mahututi kwa wiki ya tatu sasa.
Obama yuko Afrika Kusini ikiwa ni nchi ya pili Afrika kabla hajaja Tanzania siku ya jumatatu. Ziara yake iliamsha hisia kwamba Rais Obama angemtembelea Bw Mandela ambaye afya yake ni mbaya sana akiwa amelazwa akisumbuliwa na mapafu.


No comments:

Post a Comment