MWILI UMEONDOLEWA KUPELEKWA MAKABURINI
ATAZIKWA PEMBENI YA KABURI LA BABA YAKE
Kaburi la Albert Mangwea likifanyiwa maandalizi, wakati mwili ukiwa njiani kuletwa makaburini. Pembeni ni kaburi la baba yake Albert Mangwea
Wananchi wakiendelea kumiminika katika viwanja vya Jamuhuri asubui hii, uwanja huo umejaa na kusababisha shughuli ya kuaga mwili kusitishwa na msafara kuelekea makaburini.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya leo amewatukana askari wa mlangoni katika lango la uwanja wa Jamuhuri, wakati alipokuwa akijaribu kuingia uwanjani hapo bila kuwa na kitambulisho maalumu.
Dully Sykes aliwasili kiwanjani hapo asubui hii kutokea Dar es Salam ili kuaga na kuungana na wasanii wengine kutoka kona mbalimbali za nchi katika mazishi ya msanii Albert Mangwea aliyefariki dunia alhamisi wiki iliyopita nchini Afrika Kusini.
Mwili wa Ngwea unatarajiwa kuzikwa Kihonda leo pembeni ya kaburi la baba yake. Kwa sasa mwili wa Ngwea uko katika viwanja vya Jamhuri ambapo watu wengi wanazidi kumiminika katika viwanja hiyvo ili kumuaga mpendwa wao.
Mwili huo unaondoka katika viwanja hivyo sasa hivi kwaajili ya maziko. Viwanja vya Jamhuri vimejaa watu wengi kupita kiasi na kusababisha mwili kuondolewa kupelekwa makaburini
No comments:
Post a Comment