Tuesday, May 21, 2013

WHITE HOUSE YADHIBITISHA UJIO WA OBAMA




Ikulu ya Marekani ‘White House’ kupitia ofisi ya habari imetoa taarifa ya kuja kwa Rais wa Marekani nchini Tanzania. Taarifa hiyo ilidai kuwa Rais na mkewe wanategemewa kutembelea nchi tatu tu za Afrika.

Katika taarifa yake iliyotumwa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na kuwekwa kwenye mtandao wa Twitter, ilieleza ziara ya Rais Obama katika nchi za Afrika, na kuzitaja nchi hizo kuwa ni Senegal, Afrika Kusini na Tanzania. Ziara hiyo itaanza mwezi ujao (juni) tarehe 26 mpaka tarehe 3 julai.

Ziara hiyo ina lengo la kutilia mkazo umuhimu kwamba Marekani ina mahusiano mazuri na nchi zilizoka pembezoni mwa jangwa la Sahara, ikijumuisha pia na umuhimu wa kukuza biashara na uwekezaji na ukuaji wa demokrasia na uwekezaji katika viongozi wa baadae wa Afrika.

Rais atakutana na viongozi mbalimbali wa serikali, biashara, taasisi zisizo za kiserekali ambapo ni pamoja na vijana, ili kuongelea mikakati maalumu ya mahusiano kuhusiana na mambo mbalimbali ya dunia.

Safari hii ina lengo la kuongeza mahusiano na ushirikiano kati ya Marekani na watu wa nchi za Afrika katika kukuza amani na maisha salama duniani.


No comments:

Post a Comment