Tuesday, May 21, 2013

IKULU YADHIBITISHA UJIO WA RAIS WA MAREKANI NCHINI TANZANIA
                        Salva Rweyemamu, Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Ikulu

Kurungenzi ya Habari ya Ikulu imedhibitisha ujio wa Rais Obama nchini Tanzania na kutaja sababu zinazomfanya Rais Obama kuja Tanzania. Blog ya Matukio jana iliripoti taarifa za ujio wa Rais Obama ambapo baada ya kufuatilia Ubalozi wa Marekani, Afisa wake alidai, Ubalozi huo utatoa taarifa maalum wakiwa tayari.

Akizungumza kwa njia ya simu, Salva alise, Rais Obama anatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao, june 2013.

Salva alisikika asubuhi ya leo tarehe 21/05/2013 katika mahojiano na kipindi cha Jambo Tanzania katika Televisheni ya Taifa, Salva Rweyemamu alisema kati ya mambo muhimu yanayomleta Rais Obama ni pamoja na kueleza mkakati wa kusambaza nishati ya umeme ili kupambana na tatizo sugu la umeme nchini.

Salva ambaye ni Mkurugenzi wa mawasilano wa Ikulu ya Tanzania ameeleza kuwa utulivu na amani iliyopo nchini ni sababu moja wapo inayoifanya Tanzania kuheshimika na kupata fursa ya kumpokea kiongozi wa taifa kubwa kuliko yote duniani.

No comments:

Post a Comment