Wednesday, May 22, 2013

BREAKING NEWS: MTWARA KWA FUMUKA TENA LEO

Wakati hotuba ya Wizara ya Nishati na Madini inaendelea, Mtwara mjini kumechafuka na kusababisha shughuli zote kusimama, hiyo ni baada ya Waziri Sospita Muhongo
kutoa ripoti ya maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kuelekea Dar es Salaam.

Wakazi wa maeneo mbalimbali ya mji wa Mtwara wametaaruki na kuanza upya kufanya fujo kwa kuchoma matairi na kuharibu mali.

 Taarifa zisizo rasmi zilizotufikia hivi punde ni kwamba nyumba ya Mbunge na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Hawa Ghasia imepigwa mawe na kuharibika, Matukio Blog itaendelea kuwajulisha kinachoendelea Mtwara.

No comments:

Post a Comment