Wednesday, March 20, 2013

NYETI ZA WANAUME 'DILI'


HOFU imeendelea kutanda kwa wanaume kunyofolewa uume zao katika vijiji vinavyozunguka mji wa Tiringoulou, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Magharibi mwa Afrika.

Ambapo inadaiwa sehemu hizo za siri huwa zinahusishwa na imani za kishirikina kutokana na mbinu zinazotumika kutekeleza uovu huo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanyika nchini humo na baadhi ya maeneo Magharibi mwa Afrika na kuripotiwa na Shirika la Habari la Reuters juzi umebainisha hayo.

"Lilikuwa jambo la kunishangaza kwangu, kuona watu wakisalimiana kawaida mapema asubuhi baada ya kuwasili mjini Tiringoulou ambao una zaidi ya wakazi 2,000. Eneo ambalo kufika kwake ni shida ndani ya Jamhuri ya Afrika ya Kati," ilieleza sehemu ya utafiti huo.

Utafiti huo, uliongeza kuwa punde aliyekuwa anafanya utafiti husika alianza kujiridhisha kweli kuwa wanaume wananyofolewa uume zao baada ya kushuhudia tukio moja karibu na mji mmoja nchini Sudan.

"Wakati nikiendelea na safari zangu katika mmoja ya miji nchini Sudan nilishangaa kuona watu wakipeana mikono kwa asilimia ndogo, punde wanaume wawili wakanyofolewa uume zao," iliongeza sehemu ya utafiti huo.

"Nilikuwa karibu na soko ambalo watu walikuwa wanauziwa na kunywa chai. Wateja walipomaliza wakaanza kumlipa aliyekuwa anauza (mwanaume) fedha kwa kugusana mikono.

"Muuza chai punde alihisi kitu kama umeme kimepita mwilini mwake. Ghafla akajigundua uume wake umepungua ukubwa na kufikia kiwango kidogo zaidi ya mtoto, taharuki ile ilisababisha mkusanyiko pale, punde tena wanaume wawili yakawatokea kama hayo," ilifafanua sehemu ya ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, inabainisha kuwa matukio ya wizi wa sehemu za siri hususan uume wa kutoka kwa wanaume katika nchi za Magharibi na Afrika ya Kati vimekithiri.



No comments:

Post a Comment