BUSINESS TIMES
LIMETED
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
KUVAMIWA NA
KUDHURIWA KWA MHARIRI WA BUSINESS TIMES, MNAKU MBANI
AGOSTI mosi mwaka huu, Mhariri wa Gazeti la Business
Times linalotoka mara moja kwa wiki (kila Ijumaa), alijeruhiwa kwa risasi akiwa
njiani kurudi nyumbani kwake Mbagala, Dar es Salaam.
Tukio hilo lilitokea saa mbili usiku, eneo la Mtoni Madafu,
akiwa katika gari binafsi aina ya Noah inayomilikiwa na Bw. Mgeme Singili
(namba ya gari imehifadhiwa) na abiria wengine wakitokea Kariakoo kwenda
Mbagala.
Walipofika Mtoni Mtongani, gari hiyo ilisimamishwa na
majambazi sita waliokuwa katika pikipiki. Majambazi hao walichomoa funguo ya
gari na kudai wapewe begi lenye pesa kutoka kwa mmoja wa abiria waliokuwa ndani
ya gari hiyo.
Abiria waliwajibu hakuna mtu mwenye begi la pesa ndipo
majambazi hao walipoanza kufyatua risasi mfululizo (zisizo na mwelekeo),
wakiwalenga abiria ndipo moja kati ya risasi hizo ilimpata Bw. Mnaku Mbani.
Bw. Mnaku alipigwa risasi juu ya mdomo, upande wa kulia
ikatoke kwenye shavu la kushoto. Risasi hiyo iliondoa meno matatu ya juu.
Uongozi wa kampuni umezungumza na Bw. Mnaku ili kuelezea
mazingira ya tukio hilo lakini kutokana na maumivu aliyonayo, hatukuweza
kuzungumza naye kwa kirefu.
Hali ya Mnaku inaendelea kuimarika na anendelea kupata
uchunguzi wa madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Zaidi ya jeraha
hilo, Mnaku hana majeraha mengine katika mwili wake kutokana na tukio hilo.
Uongozi wa Makampuni ya Business Times Limited unaendelea
kufuatilia hali ya Mnaku kwa karibu ili kuhakikisha anapata huduma na uangalizi
unaostahili.
Taarifa Za Polisi
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, David Misime alisema
mmiliki wa gari hiyo ni mfanyabiashara ambapo uchunguzi wa polisi umebaini kuwa
majambazi hao waliamini kuwa amebeba pesa, hivyo baada ya kushuka kwenye
pikipiki walidai kupewa pesa.
Alisema katika gari hiyo watu watatu walijeruhiwa kwa
risasi akiwemo Bw. Mnaku, mwingine katika bega la kushoto na watatu alikwaruzwa
na risasi kisogoni.
Jeshi la polisi bado linaendelea na uchunguzi wa tukio
hilo na watahakikisha wahusika wote wanatiwa mbaroni haraka iwezekanavyo.
Nachukua fursa hii kuwapa pole wanahabari wote nchini,
ndugu jamaa na marafiki wote kwa tukio hilo, tuendelee kuwa pamoja na kushikamana
kuondoa uhalifu kila mmoja katika nafasi yake.
Imma Mbuguni
Mhariri Mtendaji
Majira
PICHANI
MNAKU MBANI AKIPEWA POLE NA WAFANYAKAZI WA KAMPUNI YA BTL LEO
No comments:
Post a Comment