Friday, June 08, 2012
AMUUA MKEWE KWA KUHOFIA KUBAMBIKIWA UJAUZITO
Na mwandishi wetu
MTU mmoja mkazi wa Kijiji cha Olkeijulongishu, aliyefahamika kwa jina la Bi. Neisisiri Mokoroo (25), amefariki baada ya kupigwa na mumewe kwa tuhuma za kuwa na ujauzito ambao anadai si wake.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Bw Liberatus Sabas, alisema tukio hilo lilitokea juzi katika Wilaya ya Longido Kijiji cha Olkeijulongishu kata ya
Olkeijulongishu saa 11;00 jioni.
Kamanda Sabas alisema marehemu alikutwa na mauti baada ya mume wake aitwaye Kapaito Naanjarati,kudaiwa kumshambulia mkewe wake kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyomsababishia kifo chake.
Kujibu wa taarifa za awali zilieleza kuwa tukio hilo lilitokea
baada ya wanandoa hao kwenda kwenda shambani kukata nyasi na
walipofika huko,ndipo mtuhumiwa alipomuua mkewe.
Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia na kuelekea kusikojulikana na kuwa polisi wanaendelea na msako. Kamanda Sabas alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya
Longido na uchunguzi unaendelea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment