Mshindi wa shindano la kuibua vipaji vya muziki la Bongo Star Search, ambalo sasa linaitwa Epiq Bongo Star Search atazawadiwa sh.milioni 50. Ni epiq Bongo star search baada ya kampuni ya simu za mikononi ya Zantel kutangazwa kuwa mdhamini mkuu mpya wa shindano hilo ambalo litaendelea kuonyeshwa kwenye kituo cha televisheni cha ITV.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa shindano hilo Afisa biashara mkuu wa Zantel, Ahmed Mokhles alisema kuwa mshindi wa kwanza katika shindano hilo atapata zawadi ya shilingi milioni 50 na mkataba wa kurekodi. Mbali na zawadi hiyo washiriki watakabidhiwa zawadi nyingine kutok kwa wadhamini hao wapya kwa mwaka huu,
Naye Mkurugenzi wa Benchmark Production Rita Poulsen alisema kuwa”tunatarajia kuanza kampeni za kusaka vijana mapema julai”
Alisema mikoa itakayoyumika kusaka vipaji hivyo imeongezwa mikoa nane badala ya saba kama ilivyozoeleka. Wasaka vipaji wa Epiq Bongo Star Search watakwenda Zanzibar, Lindi,Mbeya, Arusha, Tanga, Dodoma, Mwanza na Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment