Monday, February 06, 2012

Watanzania watakiwa kulinda Utamaduni

 
Kitengo cha Habari
 
Zanzibar
 
Watanzania wametakiwa kulinda na kulinda na kuheshimu tamaduni ili waweze
kusongambele na kujiletea maendeleo.
 
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni Bi.
Lily Beleko katika mafunzo kwa maafisa wa Idara mbalimbali  za serikali.
 
Akiongea kwenye mafunzo hayo Bi Beleko alisema lengo la mafunzo hayo ni kuelimisha
umma wa watanzania kulinda,kuheshinu,ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika nyanja
za kiutamaduni.
 
Akifungua mafunzo hayo Kamishna wa Utamaduni na Michezo Zanzibar bwana Hamadi Bakari
Mshindo alisema kuna umuhimu wa kulinda utamaduni na kuheshimu tamzaduni za mataifa
mengine.
 
“Kuna umuhimu wa kulinda na kuheshimu tamaduni zetu na tamaduni za mataifa mengine
lakini tuheshimu tamaduni zile zilizo nzuri pekee na kuacha tamaduni zisisoendana na
mila mna tamaduni za mwafrika”.Alisema Bwana Mshindo
 
Bwana Mshindo alisema ni wajibu kwa kila mtanzania kulinda na kuheshimmu tamaduni za
mwafrika na za mataifa mengine kwa ujumla.
Alisema mara nyingi kuna miradi mingi ya maendeleo inafanyika katika maeneo
mbalimbali lakini tamaduni za sehemu husika zinakuwa hazifuatwi.
 
Aidha alisema kwa upande wa Zanzibar wameshaanza kutoa elimu jinsi ya kulinda na
kuheshimu tamaduni za jamii mbalimbali
 
Mwisho 


No comments:

Post a Comment