Thursday, February 02, 2012

Facebook inatisha, imeingia soko la hisa kwa kishindo

Hii ni profile ya kampuni ya Facebook ilipojisajili kwenye soko la hisa Jana.

Kama inavyoonyesha mapato ya kampuni hiyo katika vitabu vyake ndani ya miaka mitatu

FB watumiaji milioni 845 kwa mwezi dunia nzima(nahisi mimi na wewe hatukosi humu), picha milioni 250 zinaingia kila siku kwenye FB, na mahusiano yaani marafiki bilioni 100, si mchezo.

Mkurugenzi wa kampuni Facebook Inc. Mark Zuckerberg

Facebook imejitosa kwenye soko la hisa Marekani ambapo imetoa ofa (IPO – Initial Public Offering) ambayo itaithaminisha kampuni kati ya dola za kimarekani bilioni 75 na bilioni 100.
Kitendo hicho kinaifanya kampuni hiyo kuwa iliyoanzishwa miaka nane iliyopita kuwa ya kwanza kwenye historia kuingia kwenye soko la hisa na kutoa ofa kubwa kiasi hicho. Lakini pia kampuni inayoendelea kukua haraka na kupata watumiaji wengi kuliko yote katika mitandao ya kijamii.
Kampuni hiyo inasemekana imeweza kuingiza pato la zaidi ya dola za kimarekani bilioni 4.27, Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya Facebook, Mark Zuckerberg, amesikika akiweka msisitizo kwenye kuendelea kukuza kampuni hiyo pamoja na mtandao wa facebook badala ya kutumia pesa itakayopatikana katika soko la hisa kwa shughuli nyingine.
Kwa mujibu wa mtandao unaoripoti habari za masoko ya hisa la The Australian, alisikika akisema Zuckerberg, ‘hatututoi huduma ili kutengeneza pesa, tunatengeneza pesa ili kutoa huduma’
Nafikiri siku hizi watu wengi zaidi hawafurahii kutumia huduma za makapuni yanayotengeneza faida bali makampuni yanayofikiria zaidi ya kutengeneza faida, aliongeza Mark Zuckerberg



No comments:

Post a Comment