Bobby Brown alikuwa jukwaani anaperfom(pichani Juu) na kundi zima la New Edition huko Mississippi masaa machache kabla ya kupokea taarifa za kifo cha aliekuwa mkewe.
Kwa mujibu wa mtandao wa Rolling Stone, Whitney Houston (pichani chini akiwa na Bobby Brown) alikutwa amekufa kwenye hoteli ya Beverly Hilton jumamosi ya jana.
jarida la US Weekly liliripoti kuwa Bobby alishindwa kushiriki kwenye nyimbo ya kwanza iliyowahusisha wenzie baada ya kupata taarifa za msiba huo, lakini baadae aliungana na kundi hilo la New Edition jukwaani ili kuendelea na shughuli hiyo.
wakatio fulani kwenye concert hiyo Bobby Brown alionekana kwenye steji akiwa na machozi na kusema "I love you, Whitney!"huku akitoa busu hewani.
Wakati anaimba nyimbo ya Tenderoni, Bobby alishindwa kujizuia na kuanza kulia huku akiomba mashabiki wake waimbe nae nyimbo hiyo.
Bobby na Whitney walioana mwaka 1992 na kuachana mwaka 2007 katika ndoa iliyoandamwa na vyombo vya habari pamoja na mashabiki kila kona. wawili hao wana mtoto mmoja anaeitwa Bobbi Kristina aliyezaliwa mwaka 1993.
Mahusiano yao yaliigizwa katika tamthiliya ya Being Bobby Brown mwaka 2005.
Whitney atakumbukwa kwa nyimbo kama Greatest Love of all, I will always love you, Count On Me, I look to You zikiwa ni baadhi ya nyimbo maarufu, pia atakumbukwa kwenye filamu ya The Bodyguard, pamoja na Waiting to Exhale
Bobby na Whitney mwaka 2001 mwezi march
Rest In Peace
No comments:
Post a Comment