Waheshimiwa mmefanikiwa kufika UHURU PEAK, pongezi zenu kwa kazi nzuri, mkawaambie wabongo ilivyo raha nao waanze kupanda mlima huo |
Kama nilivyo sema uzalendo kwanza. . . |
Hapa ni mstari mwembamba unaotenganisha usiku na asubuhi, imagine the view, sisi bado tulikuwa tunastruggle kufika Stela Point saa kumi na mbili kamili asubuhi |
Kwa wale waliobahatika kufika mtakubaliana na mimi jinsi kulivyo na mvuto wa kipekee, juu ukiwa Uhuru Peak hivi ndivyo unavyoona |
Baadhi ya wageni wakiitafuta Baranko kwa hasira baada ya kupambana na milima mawe na mabonde wakati wakiupanda mlima wa Kilimanjaro |
Uzalendo mbele, asubuhi Shira 2 jamaa wameinua bendera ya taifa kuashiria moyo wa kuendelea mbele |
Hapa jamaa wanashangaa jinsi ukungu (fog) inavyowachapa usoni maeneo ya Baranko, ni baridi we acha tu |
Hapa wadau kundi la Kilimanjaro Kiboko Climb wakiwa pamoja sharing a light moment baada tu ya kuondoka Mti Mkubwa siku ya pili kuelekea Shira 1 |
Wagumu wakijiaandaa kubeba mazagazaga ambayo yalitumika katika safari ya kuupanda mlima mrefu kuliko yote barani Africa |
Hapa wagumu wakiwa wananing'inia baada ya kukosa nafasi kwenye gari walilopanda wakati tukielekea kwenye geti la Londarosi mita 2400 toka usawa wa bahari |
Wapanda Mlima wa Kilimanjaro wakiwa katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya shughuli hiyo kufunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini(hayupo Pichani) |
No comments:
Post a Comment