Wednesday, May 18, 2011

Mtoto wa ajabu (picha inaweza kusumbua watu wengi, hivyo kuwa muangalifu)

WAKAZI wa Mombo mwishoni mwa wiki walishikwa na butwaa baada ya kumshuhudia mtoto wa ajabu (Pichani Juu) aliyezaliwa kwa njia ya upasuaji katika kituo cha afya Mombo.

Akizungumza na Dar Leo Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk.Masanja Mhezi amesema kuwa mtoto huyo alizaliwa Mei 10, mwaka huu ambapo mama yake alikuwa na maumivu makali ya tumbo pamoja na kuwa na tumbo kubwa kupita kiasi.

Amesema kuwa, baada ya kufika muda wa kujifungua mama huyo alishindwa ndipo daktari wa zamu alipoamua kumfanyia upasuaji na kumzaa mtoto huyo ambaye alikuwa na uzito wa kilo 4.

Imedaiwa kuwa mtoto huyo amezaliwa ana jicho moja baada tu ya mdomo katikati pia ana kitu kirefu  mithili ya pua cha urefu wa sentimeta nne 4 juu ya jicho moja maumbile.

Ameongeza kuwa maumbile mengine yote yalikuwa sawa isipokuwa tu alikua na meno manne chini makubwa, aliishi dakika 10 na akafariki dunia.

Amewashauri wanawake waendelee kuhudhuria kliniki pindi tu wanapohisi ni wajawazito kwani miezi mitatu ya kwanza ni muhimu kwa upimaji wa matatizo mbalimbali yanayoweza kuleta hali hiyo ikiwemo ugonjwa wa kaswende na kuepuka kumeza dawa bila ushauri wa kitabibu.

Mtoto wa ajabu ana pua juu ya jicho moja kama alivyozaliwa.


No comments:

Post a Comment