Wednesday, May 04, 2011

Matukio Mbalimbali

Jinsi picha za uongo zilivyoghushiwa kuonyesha kama Osama ameuawa. Juu kushoto ndio anayesemekana ni Osama mwenyewe, juu kulia ni picha iliyotumika kwenye matelevisheni kutangaza kuuawa kwake. chini kulia ni picha ya maiti ya mtu mwingine na katikati ni sehemu ya picha ya Osama iliyokatwa na kubandikwa kwenye maiti huyo ilikutoa picha ya kulia mwisho. Hata hivyo ikulu ya Marekani imegoma na kusema haikutoa picha zozote, Rais Obama amedai hiyo picha ni propaganda za wa tu wachache tu.

Diwani wa viti maalumu CHADEMA katika jimbo la Kawe Bi Ester akiangalia madawa hatari yaliyotupwa katika eneo la kiwanda cha Tanganyika Packers juzi, ambayo yameathiri zaid ya wakazi 200 na kupelekea wengi wao kulazwa na wengine kuishi kwa shida katika eneo hilo.

Diwani wa viti maalumu kwa tiketi ya CHADEMA, Bi Esther akiwaelezea madhara yanayoweza kusababishwa na sumu hatariinayoonekana mbele pichani iliyotupwa karibu na makazi ya watu katika eneo la Tanganika Packers, Kawe ambayo yalisababisha madhara kwa jamii yenye idadi ya watu wasiopungua 200 katika eneo hilo.

Rais wa Marekani, Barak Obama akiangalia live jinsi adui namba moja wa Marekani Osama Bin Laden akiuawa pamoja na jopo la maofisa wake katika ikulu ya Marekani maarufu kama White House, Mwanamke aliyekaa ni waziri wake wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bi Hilary Clinton.


No comments:

Post a Comment