Wednesday, March 16, 2011

Waliochaguliwa Form V 2011

Wanafunzi 36,366 wapeta, Wasichana washika mkia
Wenye umri wa miaka 25 watupwa
Dr Shukuru Jumanne Kawambwa, Waziri wa Elimu


WIZARA ya Elimu imetangaza matokeo ya uchaguzi wa kuingia kidato cha tano ambapo wanafunzi 36,366 wamechaguliwa kuingia kidato cha tano wakati kwa mwaka jana walikuwa ni 33,662.

Akitangaza matokeo hayo leo asubuhi, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Shukuru Kawambwa amesema kuwa, kwa mwaka huu matokeo yamekuwa mazuri kutokana na idadi ya wanaoingia kidato cha tano kuongezeka.

Kawambwa amesema kuwa, waliochaguliwa kwa mwaka huu wasichana ni 11, 210 na wavulana 26,156 ambapo tofauti na mwaka jana ambapo idadi ya wasichana ilikuwa ni 12,638 huku wavulana wakiwa 21,024.

Kawambwa amesema kuwa,katika uchaguzi huo wasichana 11,866 na wavulana 26,908 walikuwa na ufaulu wa daraja la kwanza hadi la tatu lakini baadhi yao hawakuwa na sifa stahili kwa kukosa sifa za daraja la tatu.

Pia amesema kuwa, wanafunzi 241 walikuwa na sifa za msingi lakini masomo waliyoyafaulu hayana uunganishi na mchepuo wa masomo yao husika.

Ameongeza kuwa, wanafunzi 29 wameachwa katika uchaguzi huo mbali ya kuwa na sifa stahili kutokana na kuwa na umri mkubwa ambao ni zaidi ya miaka 25 na kupoteza sifa za kuchaguliwa.

Habari zaidi angalia Dar Leo, fuatilia taarifa zaidi zitaendelea kuwekwa


No comments:

Post a Comment