![]() |
| Karin Mackaliunas (27) |
Baada ya kugonga gari lake siku ya jumaapili tarehe 13 mwezi machi, mwanamke mmoja jijini Scranton, nchini Marekani Karin Mackaliunas (27) alikuwa tayari kuondoka eneo la ajalia, kabla hajazuiliwa na ofisa wa polisi Anthony Cali, na kutaka azuiliwe kwa uharibifu wa mali kutokana na ajali hiyo.
Kwa mujibu wa gazeti la Scranton Times Tribune, baada ya kupekuliwa ili kuangalia kama ana silaha zozote, ndipo polisi huyo alimkuta na vipakiti vitatu vya madawa ya kulevya mfuko wa jaketi lake.
Wakati polisi huyo akimpeleka polisi kumfungulia mashtaka, alimuona akiwa amekaa kwenye gari anahangaika.
Baada ya uchunguzi na upekuzi wa kina, Mackaliunas katika hali ya kushangaza alikutwa na mifuko 54 ya madawa aina ya heroin, mifuko mingine mitupu kwaajili ya kubebea madawa hayo, na vidonge 8 kwenye sehemu za siri pamoja na kiasi cha dola za kimarekani 51.22 pamoja na chenji nyingi tu.
Kwa mujibu wa gazeti la Scranton Times-Tribune, mwanamke huyo ameshtakiwa kwa kukutwa na madawa aina ya heroin na kusafirisha madawa hayo


No comments:
Post a Comment